Thursday , 30th Nov , 2023

Baada ya hapo jana kutangazwa kwa taarifa mbaya kuhusu kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa makampuni ya ''Berkshire Hathaway'' kutokea nchini Marekani, Charles Thomas Munger

Charles Thomas Munger

 

Kijana aliyehudumu kwenye jeshi la Marekani akapigana vita vya pili vya Dunia, akaisoma sheria, akaufahamu uwekezaji na kuitamani biashara, Baba wa watoto 7; amefariki siku ya jana akiwa na umri wa miaka 99.

Mbali na yeye kumchagua rafiki ambaye waliungana kuifanya biashara haswa, ambaye pia ni Bilionea mwenzake kutokea nchini Marekani anayefahamika kama Warren Buffett, mfanyabiashara asiyechoka kuwahusia vijana kuhusu uwekezaji.

Basi fahamu yapo mambo muhimu ya kujifunza kutoka kwa hayati ''Charles Thomas Munger''

1. Usijaribu kuuza kitu chochote ambacho hata wewe mwenyewe huwezi kukinunua.
2. Usifanye kazi na mtu yoyote ambaye huwezi kumuheshimu wala kuvutiwa na yeye kwa upande wa utendaji
3. Fanya kazi na watu ambao unafurahia kufanya nao kazi.
4. Kujitambua ndiyo kila kitu kwenye maisha.
5. Usitumie zaidi ya unachoingiza (kipato)
6. Usiache kujifunza kila siku.
7. Kubali kuyapokea makosa yako.
8. Jaribu kufanya kitu kipya kila uchwao.

Chanzo: fortunemag