Thursday , 2nd May , 2024

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kuwa uzalishaji wa chakula kwa msimu wa kilimo wa 2022/2023 ulitosheleza mahitaji ya chakula ya tani 16,390,404 kwa mwaka 2023/2024 na kuwepo kwa ziada ya tani 4,011,611. 

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 2, 2024, wakati akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka 2024/2025.

Amesema kutokana na hali hiyo, Taifa limejitosheleza kwa chakula kwa asilimia 124 ikilinganishwa na utoshelevu wa asilimia 114 mwaka 2022/2023, aidha, utoshelevu wa chakula unatarajiwa kufikia asilimia 130 ifikapo mwaka 2025.