Tuesday , 3rd Sep , 2024

Mwanariadha wa Uganda Rebecca Cheptegei yuko katika hali mahututi katika hospitali moja nchini Kenya, baada ya kudaiwa kuchomwa  na moto wa petroli na mpenzi wake wa zamani.

Mwanariadha

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 33, ambaye alishiriki katika michezo ya Olimpiki ya hivi karibuni mjini Paris, ameungua kwa zaidi ya asilimia 75 ya mwili wake, polisi wamesema.

Alishambuliwa nyumbani kwake magharibi mwa Kenya, ambako alikuwa akifanya mazoezi.

Kuna wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa visa vya ukatili dhidi ya wanariadha wa nchini Kenya, baadhi yao vimesababisha vifo.