Monday , 12th May , 2025

Kimefanyika kikao cha Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na msanii Ibraah juu ya kinachoendelea kati yake na lebo ya 'Konde Gang Music' ambapo Harmonize hajatokea katika kikao hicho.

Picha ya Ibraah

Baada ya kumaliza kikao hicho na BASATA Ibraah amezungumza na waandishi wa habari anasema

"Nashukuru Mungu limefika kwenye mikono ya walezi wetu na hivi karibuni litakuwa sawa. Hii ni sheria na hii ni Serikali itaangalia wapi kuna haki".

Taarifa za awali ambazo alishea Ibraah anadai anatakiwa alipe Tsh Bilioni 1 ili aweze kutoka Konde Gang Music.