Friday , 20th Jun , 2025

Mahakama ya Kahawa Nairobi nchini Kenya imewahukumu Hussein Abdille na Mohamed Abdi Ali, waandaaji wa shambulio la hoteli ya DusitD2, kifungo cha miaka 30 gerezani kila mmoja.

Hussein Abdille alishtakiwa kwa kosa la kupanga kutekeleza kitendo cha kigaidi, pamoja na mashtaka ya kusaidia kutekelezwa kwa shambulio hilo. Mshirika wake, Mohamed Abdi Ali, alikabiliwa na mashtaka sawa ya kupanga, pamoja na mashtaka 14 ya kusaidia shambulio hilo.

Wakati hakimu alipotoa uamuzi wake mahakamani, Abdille alihukumiwa kifungo kikali cha miaka 30 kwa nafasi yake katika tukio hili la kinyama. Ali pia hakuepuka adhabu; alipatiwa miaka 15 kwa kosa la kupanga shambulio na miaka mingine 15 kwa mashtaka ya kusaidia, na kufanya jumla ya miaka 30 gerezani.

Ikumbukwe kuwa tukio hilo la kigaidi lilitokea Januari 15 mwaka 2019 ambapo watu zaidi ya 20 waliuawa #EastAfricaTV