Saturday , 21st Jun , 2025

Mwanamuziki Darassa CMG ameshea nasi taarifa ya kumpoteza mama yake mzazi na mazishi yatafanyika nyumbani kwao Itigi mkoani Singida.

Picha ya Darassa

"CMG inasikitika kutangaza kifo cha Mama mzazi wa artist Darassa CMG. Mazishi ya mwili wa marehemu yatafanyika nyumbani kwao Itigi na sio Kiwalani"

"Kwa ndugu, jamaa,rafiki au jirani ambae angependa kushiriki na sisi safari ya kwenda Itigi kumpumzisha Mama yetu mpendwa kwenye nyumba yake ya milele safari ya kuelekea Itigi itaanza leo saa 11:00 asubuhi" ameandika Darassa

East Africa TV na East Africa Radio inatoa pole kwa Darassa na familia yao kwa ujumla kuondokewa na Mama yake.