
Taarifa hii imepokewa kwa hisia mseto na mashabiki wengi waliomkumbuka Paul Walker, ambaye alifariki dunia mwaka 2013. Kurejea kwa mhusika wake kunaonekana kama njia ya heshima na kuhitimisha simulizi ya urafiki wake wa karibu na Dominic Toretto (Dom), anayochezwa na Vin Diesel.
"Tunataka kuleta hitimisho lenye heshima, ambalo litawaunganisha tena Brian na familia yake kwa njia ya kipekee." alisema Diesel katika mahojiano ya hivi karibuni.
Filamu hiyo ya mwisho inatarajiwa kutoka mwaka ujao, na tayari imekuwa gumzo mitandaoni huku mashabiki wakiwa na matarajio makubwa ya kuona familia ya Fast ikiungana kwa mara ya mwisho.