
Gamondi ataanza kazi ya kuiandaa Singida kuelekea msimu mpya wa mashindano wa 2025/26, ambapo chui hao watashiriki michuano ya ndani sambamba na kombe la shirikisho Afrika.
Wakati huohuo Kocha David Ouma na kocha Moussa N'Daw watasalia kuwa wasaidizi wa Gamond ndani ya kikosi hicho.
Gamondi aliiongoza Yanga SC kwa msimu mmoja na miezi kadhaa akitwaa Ligi kuu ya NBC, CRDB Federation Cup na kufuzu robo fainali ya ligi ya Mabingwa Afrika.