Thursday , 3rd Jul , 2025

Wahenga waliwahi kusema mbuyu ulianza kama mchicha, ndiyo wala hawakukosea ndivyo ndoto za Diogo José Teixeira da Silva kuuburudisha ulimwengu zilianza kidogo kidogo kama ambavyo mimea huota ardhini.

Kumbukumbu nzuri za Diogo Jota chini ya kocha Arne Slot katika kikosi cha Liverpool alifunga bao la kwanza la Liverpool kwenye zama za kocha huyo katika ushindi wa 2-0 walioupata Liverpool ugenini dhidi ya Ipswich Town na kumfanya kuwa namba 9 wa kutumainiwa ndani ya kikosi hiko chini ya kocha Slot.

Bao lake la mwisho ndani ya kikosi hicho alilifunga Aprili 2 katika Merseyside dabi katika ushindi wa 1-0 walioupata Liverpool ambao ni mapingwa wa EPL 2024-2025, huku mchezo wa wake wa mwisho akiwa na jezi ya timu hiyo ilikuwa Mei 25 akitokea benchi katika sare ya 1-1 dhidi ya Crystal Palace.

Pumzika kwa amani Jota, wahenga walisema mtumbuziaji mzuri huwa anafahamu wakati mzuri wa kushuka jukwaaani lakini wewe umeshuka haraka mno, wewe umeshuka bila taarifa pengine kama tungefahamu tungeomba hata EPL isiishe au basi ungetuaga pale Allianz Arena wakati ukiipatia heshima ya mwisho Ureno kwa kuwazawadia UEFA Nations League.