
Hii hapa ni orodha ya waliowahi kujutia kazi zao:
1. Oppenheimer – Baba wa bomu la atomiki. Baadaye akajuta kwa mauaji na uharibifu wa Hiroshima & Nagasaki mwaka 1945.
2. Kalashnikov – Aliunda AK-47 kwa ulinzi wa taifa, lakini alihuzunika ilipotumika kwenye mauaji ya raia.
3. Philo Farnsworth – Mvumbuzi wa luninga, alikasirishwa kuona TV ikigeuzwa burudani tupu badala ya kufanyika kuwa sehemu ya kutoa elimu kama ilivyokuwa lengo lake.
4. Ethan Zuckerman – Mtengenezaji wa Pop-up Ads, alikuja kuomba msamaha hadharani kwa “usumbufu” aliouleta mtandaoni. (Pop-up Ads - matangazo yanayokuja wakati unaperuzi kwenye wavuti mbalimbali)
5. Anna Jarvis – Alianzisha Mother’s Day kwa upendo, lakini alijuta ilipochukuliwa na wafanyabiashara kama fursa ya kuuza kadi & maua tu.
6. Wright Brothers – Walitaka ndege zisaidie usafiri wa watu, lakini zilipoanza kubeba mabomu vitani, Orville alijutia uvumbuzi wao.
Ujumbe mkubwa ‘’Teknolojia si tatizo ni matumizi yake’’