Tuesday , 22nd Jul , 2025

Mara Kadhaa msanii Rayvanny amekuwa akisahaulika ya kuwa ni miongoni mwa wasanii wakubwa kutoka Tanzania na Afrika ambao wamefanya mambo makubwa katika kiwanda cha burudani.

Haya Mambo matano (5) ambayo ameyafanikisha msanii Rayvanny ambayo yamekuwa yakisahaulika kutajwa.

1: Rayvanny ni msanii Pekee kutoka Tanzania ambaye anamiliki tuzo ya BET katika kipengele cha Viewer's choice Best New International Act ambayo alishinda mwaka 2017.

2: Msanii wa kwanza Afrika kutumbuiza katika jukwaa la Mtv Europe Music Awards (MtvEMA 2021) pamoja na majukwaa mengine makubwa Ulimwenguni.

3:Miongoni mwa Wasanii wenye kolabo kubwa kimataifa ambazo ameshirikiana na wasanii kama Gims,Maluma,NorahFatei,FerreGola na wengine wengi.

4: Msanii wa pili Tanzania kuwa na wafuasi wengi katika mtandao wa Youtube ana wafuasi Milioni 5.79, nazaidi ya watazamaji Bilioni 1.3

5: Wimbo wa Mama Tetema kuwania Tuzo za Grammy (Best Latino Pop Album) akiwa ameshirikishwa na Msanii kutoka Colombia .