Thursday , 7th Aug , 2025

Serikali ya Uingereza imetangaza mipango ya kukabiliana na biashara ya upasuaji kwa ajili ya kuboresha muenekano ikiwemo kuongeza makalio, kuongeza ukubwa wa viungo kama midomo na kuondoa makunyazi usoni.

Hatua hizo zinadhamiria kuwalinda watu walioko chini ya umri wa miaka 18 na kuhakikisha kuwa ni maafisa wa afya waliofuzu tu kuhudumu Uingereza watakaoruhusiwa kutoa huduma hizo 

Kumekuwa na wasiwasi kuwa watu wanafanyiwa upasuaji na kupewa dawa katika mazingira yasiyo salama ikiwemo majumbani, kwenye mahoteli na kiliniki za muda na hivyo kuhatarisha maisha yao. 

Baadhi ya wataalamu wanaonya juu ya uwezekano wa mgonjwa kupata matatizo, ikiwa ni pamoja na kuharibika kwa mishipa kiasi kwamba unatokea uwezekano wa mifupa kushindwa kufanya kazi tena.

   
Lakini sio suala la mwili tu : wataalamu wanaonya juu ya hatari za kisaikolojia ambazo zinapaswa kutiliwa maanani, kwani ukweli ni kwamba baadhi ya wagonjwa hawa wanaweza  hali ya - body dysmorphia- ambapo mtu hukasirishwa na muonekano wa mwili wake.