Tuesday , 12th Aug , 2025

Mahakama Kuu ya Anuradhapura nchini Sri Lanka imempata daktari mwenye umri wa miaka 70 na hatia ya kumbaka mwanamke mwenye umri wa miaka 25

Mwanamke huyo ni mama wa mtoto mmoja ambaye alikuwa amefika katika kituo cha matibabu ili kuondoa kitanzi cha uzazi ambacho kilikuwa kimepandikizwa mwilini mwake.

Hakimu ameamuru daktari mshtakiwa ahukumiwe kifungo cha miaka kumi na tano jela kigumu na mama mlalamikaji alipwe fidia ya milioni moja na nusu.

Hakimu pia amemhukumu daktari kifungo cha miaka mitatu jela ikiwa atashindwa kulipa fidia hiyo.

Baada ya hukumu hiyo kutangazwa, Wakili wa mshitakiwa, Kalinga Ravindra, aliiambia mahakama kuwa ameshangazwa na hukumu hiyo.