Friday , 5th Sep , 2025

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV amekutana hivi leo na rais wa Israel Isaac Herzog mjini Vatican.

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV amekutana hivi leo na rais wa Israel Isaac Herzog. Viongozi hao wamejadiliana kuhusu hali mbaya katika Ukanda wa Gaza.

Papa Leo XIV ametaka mazungumzo yafanyike yatakayosaidia kuachiwa huru mateka wa Israel ambao bado wanashikiliwa na Hamas na ameitisha usitishaji wa kudumu wa mapigano katika eneo hilo la Wapalestina.

Mkutano huo umefanyika wakati Israel ikiendelea mbele na operesheni iliyopangwa katika Ukanda wa Gaza na makao makuu ya kanisa hilo mjini Vatican yakihimiza usitishaji mara moja wa vita na kurejea kwa mateka waliochukuliwa na kundi la Hamas.

Afisi ya Herzog imesema kabla mkutano huo kwamba mazungumzo yalitarajiwa kutuwama juu ya juhudi za kuachiwa huru mateka, mapambano ya kutokomeza chuki dhidi ya wayahudi kimataifa na kuzilinda jamii za wakristo katika eneo la Mashariki ya Kati.