Monday , 15th Sep , 2025

Endelea kuipeperusha vyema na kuiheshimisha bendera ya Taifa letu"alisema Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amempongeza mwanariadha Alphonce Simbu kwa kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania na kufanikiwa kupata medali ya kwanza ya dhahabu kwa Tanzania katika mashindano ya dunia ya mbio ndefu yanayoendelea Tokyo nchini Japan. 

Alphone Simbu ameshinda mbio hizo  kwa kutumia saa 2:09:48 na kumshinda mpinzani wake mwanariadha Amanol Petros kutoka Ujerumani kwa tofauti ya sekunde 0.03.

"Kama nilivyokusihi uliposhika nafasi ya pili kwenye Boston Marathon mwezi Aprili mwaka huu, ushindi wako ni matokeo ya nidhamu yako ya hali ya juu na kujituma kwa bidii kwenye kazi, umekuwa mfano bora kuhusu nguzo hizo mbili za kazi kwa wanariadha na wanamichezo wenzako, na hata kwa wasiyo wanamichezo,"

Endelea kuipeperusha vyema na kuiheshimisha bendera ya Taifa letu"alisema Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan 

Kwa upande wa Wizara yenye dhamana ya michezo sambamba na Baraza la Michezo la Taifa waliofanikisha safari ya mwanariadha huyo wamepokea kwa furaha kubwa ushindi huo na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kuwa nao bega kwa bega wanamichezo wanaoiwakilisha vyema Tanzania Kimataifa.