Sunday , 28th Sep , 2025

Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Igor Klymenko amesema kuwa takriban maeneo 100 ya kiraia yameharibiwa na shambulio hilo kote nchini humo, huku vitongoji vyote vikiwa magofu.

Shambulio la anga la Urusi kwa ndege zisizo na rubani 600 na makumi ya makombora lililodumu kwa zaidi ya saa 12 limeua takriban watu wanne akiwemo msichana mdogo wa miaka 12 na kuwajeruhi wengine 70 nchini Ukraine.

Rais Volodymyr Zelensky alisema vifo hivyo vyote vilitokea katika mji mkuu, Kyiv, ambao ulilengwa na makombora mengi. Msururu huo unaohusisha takriban ndege zisizo na rubani 600 na makombora kadhaa yaliyolenga maeneo saba ya Ukraine ni mojawapo ya mashambulizi mazito zaidi katika miezi ya hivi karibuni.

Zelensky ameonya kwamba Ukraine italipiza kisasi na kusema shambulio hilo baya limeonyesha Moscow inataka kuendelea kupigana na kuua.hata hivyo Urusi kwa upande wake, imesema ilishambulia vituo vya kijeshi na makampuni ya viwanda yanayosaidia vikosi vya kijeshi vya Ukraine.

Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Igor Klymenko amesema kuwa takriban maeneo 100 ya kiraia yameharibiwa na shambulio hilo kote nchini humo, huku vitongoji vyote vikiwa magofu.

Huduma za dharura zilisema shambulio dhidi ya Taasisi ya Moyo ya Kyiv limeua muuguzi na mgonjwa. Kiwanda kikubwa cha uokaji, kiwanda cha mpira unaotumika kwenye magari, pamoja na majengo ya ghorofa na miundombinu ya kiraia pia ililengwa, kwa mujibu wa Zelensky.