Monday , 6th Oct , 2025

Lecornu, ambaye alikuwa waziri mkuu wa tano wa Macron katika kipindi cha miaka miwili, amefanya kazi kwa siku 27 pekee. Serikali yake ilidumu kwa saa 14, na kuifanya kuwa ya muda mfupi zaidi katika historia ya Ufaransa.

Waziri Mkuu mpya wa Ufaransa Sebastien Lecornu na serikali yake wamejiuzulu mapema leo  Jumatatu, saa chache baada ya Lecornu kutangaza orodha yake ya baraza la mawaziri, katika hali inayozidisha mzozo wa kisiasa wa Ufaransa ambao umesababisha kushuka kwa hisa na euro.

Kujiuzulu kwa haraka na kusikotarajiwa kumekuja baada ya washirika kutishia kuiangusha serikali mpya.
Kufuatia hatua hiyo, mkutano wa kitaifa wa siasa kali za mrengo wa kulia umemtaka Rais Emmanuel Macron kuitisha uchaguzi wa haraka wa bunge mara moja.

Lecornu, ambaye alikuwa waziri mkuu wa tano wa Macron katika kipindi cha miaka miwili, amefanya kazi kwa siku 27 pekee. Serikali yake ilidumu kwa saa 14, na kuifanya kuwa ya muda mfupi zaidi katika historia ya Ufaransa .

Lecornu akielezea kwa nini hakuweza kuendelea na kufanya maelewano na vyama pinzani, amelaumu ubinafsi wa wanasiasa wa upinzani. Wakati huohuo Deni la Ufaransa limepanda hadi 113.9% ya pato la taifa.