Friday , 17th Oct , 2025

Mama wa watoto 3 na rapa wa kike Marekani Cardi B, amewashauri wanawake watafute pesa zao wenyewe hata kama watakuwa na wanaume wenye pesa.

Picha ya msanii Cardi B

Moja ya Interview aliyofanya Cardi B anasema Mwanamke ana jukumu la kumiliki pesa zake, kujipa majukumu na ku-hustle ili kupata chake binafsi.

"Kama mwanamke hata kama umepata mwanaume mwenye pesa unatakiwa uwe na zako binafsi, inakuwa haina haja ya kumwambia mwanaume afanye vitu kwa ajili yako".

"Hustle zako, majukumu yako, jitahidi uweze kupata cha kwako" - Cardi B

Kwa upande wake hakuna mtu aliyempa chochote, alifanya kazi kwa bidii na kuwekeza pesa zake kwenye kazi yake ya muziki.

Huenda ukweli huu wa Cardi B unaweza usipendwe na baadhi ya wanawake wengi Africa hasa Tanzania, ndani ya mkoa Dar es Salaam