
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametangaza siku ya Jumatano Oktoba 29, kuwa ni Siku ya Mapumziko kwa Wananchi wa Zanzibar kutokana na kuwa ni siku ya Uchaguzi Mkuu.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Zanzibar imesema kuwa uamuzi huo unalenga kuwapa nafasi Wananchi wote wenye sifa kwenda kupiga Kura ili kutekeleza wajibu wao wa Kidemokrasia.
Kupitia taarifa hiyo, wananchi wote wameombwa kufuata maelekezo na miongozo iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ili kuhakikisha zoezi la upigaji kura linafanyika kwa amani, utulivu na nidhamu.