Thursday , 20th Nov , 2025

Katika hatua muhimu ya kuelekea upatanishi na uwazi wa kitaifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezindua rasmi Tume Maalum ya Kuchunguza Ghasia na Vurugu zilizojitokeza nchini kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Uzinduzi huo unaashiria dhamira ya serikali kupata majibu ya msingi kuhusu matukio yaliyotikisa amani ya nchi na kusababisha migogoro ya kisiasa.

Akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa Tume hiyo, Rais Samia alisisitiza wajibu mkuu wa Tume: kufukua mizizi ya matatizo. Alitaja maswali ya msingi ambayo Watanzania wanataka yajibiwe.

"Tume tunaitarajia ikatuangalizie, sababu hasa iliyoleta kadhia ile sababu hasa ni nini? Kiini cha tatizo ni nini?" - Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania.