Tuesday , 16th Dec , 2025

Ikiwa ni ziara yake ya kwanza nchini Ethiopia, Modi atatumia siku mbili huko Addis Ababa, kwa mwaliko wa mwenzake wa Ethiopia, Abiy Ahmed.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi anafanya ziara ya Kiserikali nchini Ethiopia leo Jumanne hii, Desemba 16 wakati India ikijaribu kuongeza ushawishi wake katika bara la Afrika.

New Delhi imebaini kwamba Ethiopia ambayo ni makao makuu ya Umoja wa Afrika na mwanachama wa BRICS+, itaipatia faida kadhaa ambazo zinaweza kutumika kama msingi katika mkakati wake wa kuashiria nguvu barani Afrika ikiwemo faida ya akiba kubwa ya elementi adimu za ardhi na madini muhimu ambayo hayajatumika.

Ikiwa ni ziara yake ya kwanza nchini Ethiopia, Modi atatumia siku mbili huko Addis Ababa, kwa mwaliko wa mwenzake wa Ethiopia, Abiy Ahmed.

New Delhi inaiona Ethiopia ikiwa na umuhimu wa kiuchumi na kijiografia katika bara la Afrika, ambapo India inakusudia kuongeza ushawishi wake, hususani dhidi ya China.

Kiuchumi, India inaiona Ethiopia kama nchi yenye ahueni. Tayari zaidi ya makampuni 175 ya India yanafanya kazi nchini Ethiopia, hasa katika sekta ya nguo.

Wakati Ethiopia ikijitahidi kuvutia uwekezaji zaidi wa India hasa katika sekta za dawa, usindikaji wa kilimo, na kampuni ndogo na huku India pia ikilenga kufikia soko la Afrika kupitia Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika (AfCFTA), ziara ya Narendra Modi nchini Ethiopia inatarajiwa kuhitimishwa kwa makubaliano kadha.