Thursday , 18th Dec , 2025

"Hebu tuone aibu kama hii changamoto tunaisababisha sisi halafu tunakutana kujadiliana tutaitatuaje, inabidi tuanze sisi wenyewe" .

Kufuatia mgogoro wa wakulima na wafugaji Kiteto unaogukuta kimya kimya na kutishia usalama wa pande hizo haswa kwa jamii ya kifugaji maasai baada ya kusalitiana kwenye maeneo waliyotenga kwa shughuli za ufugaji, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Ng'wasi Kamani amelazimika kuingilia kati na kutoa msimamo wa Wizara hiyo.

Akizungumza na mamia ya wafugaji wa Kijiji cha Orkitikiti, Lerug, Engang'uengare, na Ngapapa vinavyounda nyanda ya malisho ya Olengapa Waziri Kamani ameonya wanaolima sehemu hiyo akiapa kuwalinda wanaotetea nyanda hiyo isiharibiwe.

"Hebu tuone aibu kama hii changamoto tunaisababisha sisi halafu tunakutana kujadiliana tutaitatuaje, inabidi tuanze sisi wenyewe" amesema.

Amewataka wakulima waliokodisha maeneo ya nyanda ya malisho ya Olengapa kuondoka pasi na kulazimishwa kwani awali walikutana vijiji vinne na kutenga maeneo hayo ili yawasaidie kwa shughuli za ufugaji, wazo ambalo liliungwa mkono na Serikali.