Tuesday , 17th Feb , 2026

Legend na staa wa muziki zamani 'Mr Nice' amemjia juu Dudubaya kwa kitendo cha kumtukana mtoto wake mbele ya Camera akidai msanii huyo akili zake haziko timamu.

Picha ya Dudubaya na Mr Nice

"Huyu mtu wenu anayejiita Dudubaya akili zake sio timamu, unawezaje kumtukana mtoto wako mbele ya camera? na unajiita konk master na ulipigwa na kikosi cha mizinga".

"Sikatai ulinitegua kiuno lakini na wewe baada ya kunivunja kiuno ukapigwa na kuvuliwa nguo mbele za watu" ameandika Mr Nice.

Wawili hao Mr Nice na Dudubaya hawana uhusiano mzuri tangu zamani sababu ya ugomvi wao wa muda mrefu wa kimuziki.