Monday , 17th Mar , 2014

Timu ya Viongozi wa Shirikisho la Wasanii Tanzania, leo hii wameenda kumuona msanii wa muziki Noorah a.k.a. Baba Stylz ambaye kwa sasa anaugua maradhi ya tumbo ambayo yamesababisha kulazwa hospitali kwa muda.

Timu hii ikiongozwa na Samuel Mbwana wametumia nafasi hii pia kuwasilisha mchango kidogo kwa msanii huyu ili kusaidia gharama za hapa na pale wakati huu ambapo msanii huyu anaendelea kupona.

Noorah aliripotiwa kusumbuliwa na tatizo la utumbo kujikunja ambapo alifanyiwa upasuaji kwa ajili ya kulitibu tatizo hili ambalo kwa mujibu wa wataalam, lingeweza kumgharimu maisha yake endapo angechelewa kuchukua hatua za matibabu.

eNewz imeongea na kiongozi wa msafara huu ambaye alikuwa na haya ya kusema: