Mwanamke ajeruhiwa kwa risasi Sinza
Mwanamke aitwaye Mariam mkazi wa Sinza Lion Dar es Salaam, amejeruhiwa kwa kupigwa risasi maeneo ya begani katika harakati za Polisi kuwatuliza raia wenye hasira kali waliokuwa wanataka kumpiga mwizi aliyekwapua simu kwenye bodaboda majira ya saa 12:00 asubuhi ya leo Mei 20, 2022.