Waziri Mkuu akagua nyumba za wanaohama Ngorongoro

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa madarsa ya Shule ya Msingi katika kijiji cha Msomera wilayani Handeni Mkoa wa Tanga kwa ajili ya wananchi walioridhia kuhama katika Hifadhi ya Ngorongoro kwenda kujishi katika kijiji hicho, Aprili 24, 2022. Kulia kwake ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga na na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuendelea kusimamia kwa ukaribu na kuhakikisha shughuli za ujenzi katika kijiji cha Msomera kilichopo Handeni Makoani Tanga zinakamilika haraka.