Bibi amuua mjukuu kwa maji ya moto kisa kujisaidia
Mtoto mwenye umri wa miaka minne mkazi wa Kijiji cha Lyabukande, Halmashauri ya Shinyanga amefariki dunia baada ya kupigwa fimbo na bibi yake kisha kumwagiwa maji ya moto kutokana na kujisaidia hovyo huku mdogo wake mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu akijeruhiwa kwa fimbo.