Mchungaji auawa kisa milioni 2
Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa linamshikilia Naftali Lulandala, mkazi wa kijiji cha Uhambingeto kwa tuhuma za mauji ya mchungaji wa KKKT dayosisi ya Iringa (Pichani) Elizabeth Amos, baada ya kuingia tamaa ya fedha na kumpora marehemu huyo kiasi cha shilingi milioni 2 kabla hajamuuwa.