Spika Ndugai aagiza NIDA waitwe na kieleweke
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, ameiagiza kamati ya mambo ya nje ya ulinzi na usalama ya Bunge hilo, kuwaita Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), ili kuwahoji na kujua sababu inayokwamisha kasi ya utaoji wa vitambulisho vya Taifa kwa wananchi.