Simba SC watamba usiku wa tuzo za TFF
Mabingwa watetezi wa ligi kuu, klabu ya Simba imefanikiwa kuzoa tuzo nyingi, tuozo 6 kwenye hafla ya utoaji tuzo ambayo ilifanyika usiku wa jana Oktoba 21, 2021 kwenye ukumbi wa Mwl JK Nyerere Jijini Dar es salaam. Yanga iliondoka na tuzo 2 ilhali Azam, Coastal na Mbeya City walipata moja.