Askari walioomba rushwa ya Mil. 100 wafukuzwa kazi
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo
Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha limewafukuza kazi kwa fedheha askari wanne na kuwasimamisha kazi wakaguzi wawili wa polisi ambao wanatuhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni 100.