Jen. Mabeyo asikitishwa na vijana 854 waliogoma
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jen. Venance Salvatory Mabeyo ameeleza kusikitishwa kwake na vijana 854 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambao wamekiuka taratibu kwa kuanzisha mgomo na kufanya maandamano ya kwenda Ikulu kutaka kumuona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu.