Simba yaisogelea Yanga kileleni
Mabingwa wa Tanzania bara Simba SC imepanda mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo uliochezwa jioni ya leo katika dimba la Mkapa Dar es salaam.