Pirlo kufutwa kazi na Dybala kusepa Juventus ?
Uongozi wa klabu ya Juventus ya Italia kupitia makamu mwenyekiti wake Pavel Nedved umesema bado wanaimani na kocha wake wa sasa Andrea Pirlo licha ya klabu hiyo kuonekana kuanza kuyumba kwenye mnio za ubingwa wa Serie A na kuondoshwa na FC Porto kwenye ligi ya mabingwa Ulaya.