Wanawake Mara wafungishwa ndoa na makaburi
Baadhi ya wanawake wilayani Serengeti mkoani Mara, wamelalamikia uwepo wa mila kamdamizi ya kuozeshwa mwanaume aliyefariki dunia maarufu kama ndoa ya makaburi jambo ambalo linawanyima haki na uhuru wa kuchagua mwanaume hivyo kufanya wanawake kuendelea kukandamizwa.