
Wanawake Perepetua Njiku (Kushoto) na Christina Samwel
Wakizungumza na East Africa Television kwa nyakati tofauti, wanawake hao wamesema kuwa unakuta mtu ameshafariki dunia siku nyingi lakini jamii inalazimisha kwamba yule aliyefariki dunia awe na familia na kukuza ukoo licha ya kwamba alikwishatangulia mbele za haki siku nyingi na kuiomba serikali iingilie kati.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu, amesema kuwa wanawake wengi wilaya ya Serengreti wanafanyiwa ukatili wa kijinsia na wananyamaza kimya.
Ndoa za makaburi ni maarufu kwa baaadhi ya makabila yaliyopo mkoani Mara, ambapo mwanaume anapofikia umri wa kuoa akafariki basi familia humuozesha mke ambaye akizaa watoto wanaitwa kwa jina la merehemu na dio maana zinaitwa ndoa za makaburi.