Waganga waomba dawa zao zianze kutumika hospitali
Baadhi ya waganga wa tiba asili mkoani Mtwara, wameiomba serikali kuthamini mchango wao huku wakilalamikia suala la usajili na kuomba kuruhusiwa kupeleka dawa zao zilizothibitishwa kutumika hospitalini ili kuokoa maisha ya watu hasa wenye matatizo ya upumuaji.