Kituo cha mabasi Mbezi Luis kuanza kutumika Feb 25
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Aboubakar Kunenge amesema ifikapo Alhamis ya Februari 25 kituo kipya cha mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi cha Mbezi Luis kitaanza rasmi kutoa huduma na kituo mabasi Ubungo kilichokuwa kikitumika awali hakitotumika tena.