Jafo atamani stendi ya Mbezi iitwe Magufuli
Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo, amesema kuwa kutokana na stendi mpya ya mabasi ya Mbezi Luis kuwa na hadhi ya kimataifa, anapendekeza ipewe jina la Rais Dkt. Magufuli, kama seemu ya shukrani na kuthamini jitihada alizofanya na kwamba atamuomba ili aridhie ombi hilo.