DC atoa neno walinzi waliompiga anayeuguza mgonjwa
Mkuu wa wilaya Shinyanga, Jasinta Mboneko, ameuagiza uongozi wa kampuni ya ulinzi ya Suma JKT, kuwachukulia hatua kali za nidhamu walinzi waliohusika kwenye tukio la kumpiga mwananchi Daudi Lefi, aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa huo kumuhudumia mgonjwa.