Majaliwa awasimamisha vigogo wawili Bandarini
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Bi. Nuru Mhando pamoja na Meneja wa matumizi ya fedha wa TPA, Bi. Witness Mahela ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha zinazowakabili.