Waziri akiri soka linaipaisha Tanzania duniani
Mchezo wa mpira wa miguu unaongoza kuwa na wachezaji wengi wanaocheza nje ya nchi, ukilinganisha na michezo mingine, na Tanzania inajumla ya wanamichezo 54 wanaocheza michezo ya kulipwa nje ya nchi, hii ni kwa mujibu wa Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo Mh. Innocent Bashungwa.