CHADEMA yatoa siku 2 kwa Halima na wenzake
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetoa siku mbili kwa wanachama wake 19, ambao jana walikula viapo Bungeni vya kuwa wabunge wa viti maalum bila ridhaa ya chama kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha kamati kuu ya chama hicho kitakachofanyika Novemba 27, 2020.