Afungwa miaka 30 kwa kukutwa na bangi
Mkazi wa Kijiji cha Majengo, Kata na Tarafa ya Mtama, Wilaya ya Lindi Ramadhani Haji Juma, amehukumiwa kwenda gerezani kutumikia kifungo cha miaka 30, baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na madawa ya kulevya aina ya Bangi yenye uzito wa Kilo 7.8 kinyume cha sheria.