Bei ya mifuko mbadala yazidi kupaa sokoni
Wafanyabiashara wa soko la Manzese lililopo Manispaa ya Morogoro wameiomba serikali kuzalisha kwa wingi mifuko mbadala kwani upatikanaji wake kwa sasa ni mdogo huku bei ikizidi kupaa, hali inayopelekea wateja kushindwa kumudu kuinunua.