Mechi ya kwanza, Amri Said aitoa mkiani Biashara
Kocha mpya wa klabu ya soka ya Biashara United ya Mara, Amri Said maarufu ‘Stam’ ameanza vizuri maisha yake mapya ndani ya klabu hiyo baada ya kuiongoza timu yake kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Mbeya City.