Chirwa ahesabiwa masaa Azam FC
Usajili wa mshambuliaji wa Azam FC, Obrey Chirwa sasa umekamilika kwa asilimia 100 baada ya kupatikana kwa Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) kutoka shirikisho la soka nchini Misri (EFA) ambako alikuwa akicheza awali kabla ya kusajiliwa na wanalambalamba hao.