JPM asisitiza kiongozi mwenye kujali wanawake UWT
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wajumbe wa Baraza Kuu wa Umoja wa Wanawake CCM (UWT) kuchagua kiongozi ambaye atakuwa anajali wanawake na siyo kujali tumbo lake.