Pointi 3 zinatosha kutetea ubingwa - Mwambusi
Kocha msaidizi wa mabingwa watetezi Ligi kuu Tanzania Bara Young Africans, Juma Mwambusi amefunguka kwa kujitapa kuwa mechi ya kesho dhidi ya Kagera Sugar watahakikisha wanaondoka na ushindi wa pointi 3 licha ya wapinzani wao kuwa na uwezo mkubwa.