El Maamry kuhitimisha sakata la Kessy wiki hii
Msuluhishi wa kisheria wa sakata la madai ya Simba dhidi ya Young Africans kuhusu mchezaji Hassan Kessy, Wakili Mzee Said El-Maamry anatarajiwa kukutana na pande zinazopingana Alhamisi Novemba 3, mwaka huu ili kufikia mwafaka wa mwadai hayo.